SOMO: MWANAMKE NA KANISA
UFUFUO NA UZIMA PUGU
MAMA YETU: GLORY GWITEGO
TAREHE: 9/3/2025
SOMO: MWANAMKE NA KANISA
Mwanzo 2:23
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
- mwanamke ni msaidizi katika eneo alilowekwa kutenda kazi, kwenye ndoa ni msaidizi wa mume wake.
Waamuzi 13:2-5
2. Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani jina lake akiitwa Manoa na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
3. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
4. Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi
5. kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na wembe usipite juu ya kichwa chake maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
-Yawezekana ukawa tasa wa kiroho, tasa wa uzao wa kimwili, tasa kiuchumi lakini leo Bwana atafanya jambo jipya katika maisha yako. Yale uliyo lilia kwa muda mrefu Bwana anakupa jambo jipya katika maisha yako amka tena usilie, yawezekana mambo yako yamelala Bwana anaenda kuyaamsha tena.
-Mwanamke unaweza ukapita katika mapito ambayo uwezi kumweleza mtu yoyote lakini Mungu anajua wakati wa kukujilia.
-Tunapo takiwa ni kukaa na kumsikiliza Mungu, utakapo kaa na kusikiliza Mungu ataachilia ujumbe au neno kwa ajili yako yaitaji utulivu wa rohoni na mwilini ili kuweza kusikia ni kitu gani Mungu anaongea nasi.
-Mwanamke ukitulia Bwana atasema, Bwana atatenda katika kila eneo yatupasa kutulia. Yawezekana umepitia katika dhiki na mateso baba yetu ajanyamaza ipo siku atatenda.
Waamuzi 4:4
4. Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
-Tunaona kuwa mwanamke anaenda kukabili jeshi la maadui zake kwakuwa anaamini Bwana yupo upande wake, usiogope walivyo navyo juu yako amini tu kuwa Mungu anakusudi na maisha yako akiwa ndani yako hawezi kukuacha.
Ester 4:15-17
-kuna mahali unataka kwenda lakini unaogopa, jitie nguvu nenda kwa ujasiri na ushujaa na mkono wa Mungu utakufanikisha
-ukishamjua adui yako usimwonyeshe hasira yako kwa nje ila utende kwa hekima na akili ili ummalize
Post a Comment