SOMO: ALIPATA KUTOKEA NDOTONI.
UFUFUO NA UZIMA PUGU
BABA YETU: ELDADI GWITEGO
TAREHE: 16/3/2025
SOMO: ALIPATA KUTOKEA NDOTONI.
-Mungu ili atuvushe huwa analituma neno lake. Kama hivu tunavyo jifunza kuwa alipata kutoka ndotoni tunajifunza kuwa Mungu anatuma neno lake kupitia ndoto kujulisha kuwa mtu amepata.
-Dunia imesukwa kwamba kila mtu anae mkiri Yesu basi atakuwa ni mtu wa kupingwa kwa kila kitu anacho kifanya, ila Yesu amekuja kupindua kile kilicho batilishwa na shetani.
-ili kuushinda ulimwengu huu unaotawaliwa na shetani na mawakala zake ni lazima tujikite haswa katika kumcha Mungu ili tuweze kuvuka
Mwanzo 1: 26
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
-Kila mmoja kuna kitu ameandaliwa atawale, na amiliki. Baraka inasababisha kile ucho kusudiwa kwa baraka hiyo kitimie, kifunguke kije.
-Lakini laana kazi yake ni kuzuia baraka aliyi barikiwa mtu.
-Kumiliki kunatokana na kufata neno la Bwana, kufuata neno la Bwana, kusimamia neno la Bwana na kutenda/kutuu yale ya Bwana.
-Tunatakiwa kuamka na kujipanga kama vile Mungu alivyo tusuka ili tuweze kuwa wamiliki na watawala. Amka sasa usonge mbele kuendea hatima yako kuendea kesho yako.
-Wokovu ni wa mmoja ili kuweza kupenya katika kesho yako, mashetani wako kwa ajili ya kuzuia kesho yako ila ukiamua kuamka sasa na kuiendea kesho yako majini na mashetani ya ukoo lazima yapishe ili wewe uweze kuiendea kesho yako.
-Unapaswa wewe uuongoze mwili wako lakini siyo mwili ukuendeshe wewe kwa sababu wewe ni roho kutoka mbinguni ili uweze kutimiza kusudi la Mungu hapa duniani.
-Ili wewe uweze kumiliki Mungu hukuletea ndoto juu ya miliki yako. Ndoto izo ni Mungu anakwambia unacho takiwa kumiliki. Na unapo oto akili yako inatakiwa ibadiriki na kufunguka kutokana na kuelewa juu ya ndoto kuwa ndoto ni ujumbe kutoka kwa Mungu.
1 wafalme 3:4-15
4. Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
5. Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.
6. Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
-Unapaswa kupiga hatua haijarishi ni vikwazo vingapi utakutana navyo ila katika iyo safari mbeleni muujiza wa Mungu lazima utatokea kukuokoa.
-ukiona unaingia kwenye tabu usifikiri Mungu amekuacha wewe endelea kusonga mbele utaona mkono wa Mungu ukikuokoa.
Post a Comment