SOMO: NIMEPEWA LAKINI VINAMILIKIWA.

UFUFUO NA UZIMA PUGU


BABA YETU: ELDADI GWITEGO


TAREHE: 23/2/2025


SOMO: NIMEPEWA LAKINI VINAMILIKIWA.


-Mungu anaweza kukupatia kitu lakini kuna mamlaka nyingine ikakichukua na kukimiliki 

ziko mamlaka zinazoteka na kutawala vitu walivyopewa wana wa Mungu.


Yoshua 6:1

1. Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 

2. Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. 


-Kuna chakwako ambacho umeshapewa ila wewe upande mwingine unaona kumesha fungwa, ila katika ulimwengu wa Mungu anajua ushapata teyari. Katika biashara, kazi, mtaji. 


-Mungu anaweza akwa amekuhaidi kitu ila mamlaka za giza zikawa zinakilinda kitu kilekile ambacho Mungu amekupa.


-Ikiwa Mungu ameshakupa haijalishi watafunga na kushikiria kwa muda gani ila Bwana wa majeshi atahakikisha unakipata kwa jina la Yesu. 


1. Usiogope kwa sababu hauoni njia amini umepewa


2. Usiogope kwa sababu unaona mwili unauma amini umeshapewa


3. Usiogope kwa sababu huoni dalili ya kuvuka shida yako amini umeshapewa.


4. Usiogope kwa sababu ya magumu unayo pitia amini umeshapewa.


-Hatuenendi kwa sababu ya jinsi tunavyo ona bali tunaenenda sawa sawa na Bwana alivyo sema. Yale maisha uliyo taka ameshakupatia.


-Ukiangalia jambo lako kama lilivyo fungwa utabaki kama ulivyo, ila ukiliangalia kwa namna ambavyo Bwana anasema basi utapokea sawa sawa na Bwana alivyo sema. 


-Ni kweli mazingira yanaonyesha vimefungwa lakini Bwana haangalii hali ilivyo wala muonekano ulivyo alilo lisema lazima litatimia. Simamia neno endelea kwenda.


-Mungu ni Mungu wa kila mtu. Ukisimama na neno la Bwana ukiwa unaenda atakae kuwa anapambana na wewe atakuwa anashindana na Bwana pasipo yeye kujua na ashindanae na Bwana ameshapondwa kabisa.


-Yuko Yesu pamoja na wewe, yuko Mungu pamoja na wewe endelea kusonga mbele kulekule waliko watashangaa jinsi vile unavyo pandishwa shuu sawa sawa na mapenzi ya Mungu.


Yoshua 14: 6-15

Yoshua 15: 13-17



Matendo 13: 1-6

1. Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. 


6. Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu 


Adui anamkwamisha yule anayeshugulikia mambo yako ili wewe ukwame

See Also :