SOMO: KUONGOZWA NA ROHO WA MUNGU
*UFUFUO NA UZIMA PUGU*
*BABA YETU: ASKOFU ELIDADI GWITEGO*
*TAREHE: 19/01/2025*
*SOMO: KUONGOZWA NA ROHO WA MUNGU*
- mwana wa Mungu ili atembee vizuri katika ushindi ni lazima aongozwe na roho wa Mungu.
- mwana wa Mungu asipoongozwa na roho wa Mungu atakwama, lakini roho akipata nafasi ndani yake atashinda.
NAMNA AMBAVYO ROHO WA MUNGU HUONGOZA WANA WAKE
*LUKA 4:1*
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
- Roho ana uwezo wakuongoza wana wa Mungu
- Roho wa Mungu Huwa anaongoza watu kwenye mapenzi ya Mungu
*YOHANA 16:13*
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
- Roho wa Mungu anaongoza wana wa Mungu katika kweli yote
- Roho wa Mungu huwapasha habari wana wa Mungu kwa habari ya mambo yajayo.
*WAKOLOSAI 3:15*
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani
- Roho wa Mungu humpa mwana wa Mungu amani ndani ya moyo wake ili imsaidie kuamua katika maamuzi yaliyo mbele yake.
*MWANZO 3:8-9*
Mwanzo 3:8-9
[8]Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
[9]BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
- Mungu huwaongoza wana wake kwa sauti yake.
*ISAYA 55:8-9*
[8]Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
[9]Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
- Roho wa Mungu huongoza Wana wake kwa kutumia mawazo, huwapa wana mawazo yake namna yakutenda katika maisha yao.
*MATENDO 13:1-2*
[1]Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.
[2]Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
- Roho wa Mungu huongoza wana wake katika maombi
*EZRA 6:14*
Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi.
- Roho wa Mungu huongoza wana wake kwa kupitia mahubiri ya watumishi wake.
- mahubiri humtengeneza mtu humfanya aamke tena ajitie nguvu mpya katika Bwana ili asonge mbele.
*MAOMBI*
kuomba kuongozwa na Roho katika maisha yetu, ili Roho atuongoze namna ya kushinda na kuvuka na kusonga mbele
Post a Comment